Sunday, June 2, 2019

UFUNGUZI WA MASHINDANO YA PROPHET SUGUYE CUP 2019

 Chief Prophet Dk. Nicolaus P. Suguye Muanzilishi na Mdhamini wa Michuano ya Prophet Suguye Cup 2019 akiwa na Mratibu wa Mashindano Robert B. Mujuni, Mratibu Msaidizi Martin Mwesiga, Muinjilisti Mkuu Anna Suguye, Nabii Anthony wakiingia uwanjani (Misitu-Kivule)

Tuesday, September 26, 2017

USINDIKAJI WA PAPAI

USINDIKAJI WA PAPAI
Papai ni mojawapo ya mazao ya matunda yenye vitamini A na madini ya kalishamu kwa kiasi kikubwa sana.
Zao Hili hustawi kila mahali nchini Tanzania. Kwa mwaka, wastani wa tani 2,580 hadi mwaka 2016, huzalishwa kote nchini, na uzalishaji wa zao hili unaongezeka kila msimu kulingana na uhitaji.

Matunda husindikwa ili kupata bidhaa za aina mbalimbali kama vile jamu, na matunda makavu.

NAMNA YA KUSINDIKA PAPAI ILI KUPATA JUISI
Mahitaji:
Visu vikali visivyoshika Kitu
Vyombo vya kuoshea matunda
Mashine ya Kusaga matunda
Kipimo cha Sukari
Chupa zenye mifuniko imara
Saa
Nembo na lakiri 
Kipima joto
Sufuria
Jiko
Mwiko
Vitambaa au chujio

MALIGHAFI KWA AJILI YA KUTENGENEZA LITA 3 ZA JUISI
MAPAPAI mawili ya ukubwa wa kati
Sukari gramu 100
Juisi ya limao/ndimu kikombe cha Chai kimoja
Maji safi na salama Lita 3

NAMNA YA KUSINDIKA
Osha matunda kwa maji safi na salama
Menya kuondoa Mabanda na mbegu
Katakata vipande vidogo vidogo, kisha saga kwa kutumia mashine ili kupata rojo.
Ongeza maji ya limao au ndimu ili kupata ladha. Katika Kila Lita 1 ya rojo ya mapapai weka kikombe kimoja cha Chai cha Juisi ya limao au ndimu ili kuongeza ladha na kuboresha uhifadhi. Ongeza maji safi kiasi cha Lita 3.
Chuja kwa kutumia chujio safi.
Chemsha mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 20 ukiwa unakoroga katika joto la nyuzi 80°C hadi 90°C 
Ipua
Weka Juisi kwenye chupa safi zilizochemshwa Ikiwa na moto kisha funga kwa mifuniko imara.
Panga chupa kwenye sufuria kisha weka weka maji kufikia nusu ya kimo cha chupa.
Chemsha chupa kwa muda wa dakika 20 ili kufisha bakteria na vimelea vinginevyo.
Ipua chupa na acha zipoe
Weka nembo
Hifadhi katika sehemu safi yenye hali ya joto lisilozidi nyuzi 25°C na isiyo na mwanga mkali.

MATUMIZI
Juisi hutumika kama kinywaji au kiburudisho na ina virutubisho vya vitamini C na A kwa wingi

USINDIKAJI WA MAPAPAI KWA KUKAUSHA
Mahitaji:
Kaushio bora
Mashine ya kufungia, au jiko la mkaa, au mishumaa.
Meza safi ya Kukutia
Kisu kisichoshika Kitu
Beseni la kuoshea
Mifuko ya plastiki au chupa ya plastiki au kioo.

MALIGHAFI
Mapapai yaliyoanza kuiva
Maji ya malimao au ndimu

JINSI YA KUTENGENEZA
Osha mapapai yaliyoiva vizuri na yasiyo na magonjwa wala mikwaruzo.
Menya kwa kutumia kisu kikali kisichoshika kutu.
Katakata kwenye kipande visivyozidi urefu wa sentimita 10 na Unene wa milimita 3. Ujizidisha ukubwa wa vipande havitakauka vizuri na kusababisha ubora wake kushuka.
Viweke vipande hivyo ndani ya maji ya malimao au ndimu kwa muda wa dakika 1 hadi  2 ili kudumisha rangi papai na kuongeza ladha.
Panga vipande kwenye trei za kaushio
Kausha kwa muda wa siku 3 hadi 4 kutegemeana na hali ya jua.
Fungasha kwenye mifuko ya plastiki au chupa za kioo safi na uhifadhi kwenye sehemu kavu nyenye mwanga hafifu na safi.

MATUMIZI YA PAPAI
Papai lililoiva
Huliwa kama tunda
Hutengenezwa Jamu na Juisi
Hukaushwa na Kuliwa kwa kuchanganywa wenye saladi ya matunda au keki.
Hutia ladha kwenye ice cream

Papai bichi
Utomvu wa papai bichi, hutumika katika matumizi yafuatayo;
Kutengeneza peremende, dalia, urembo, na madawa ya kulainisha Tumbo.
Huwekwa kwenye nguo wakati wa kutengenezwa ili isifupike.
Hulainisha nyama.
Hulainisha ngozi.

Papai bichi pia hutengenezwa
Mboga
Achari
 


 

MAELEZO YA MSINGI KUHUSU KILIMO CHA VITUNGUUMAJI

MAELEZO YA MSINGI KUHUSU KILIMO CHA VITUNGUUMAJI

Vitunguu ni zao la mbogamboga na hulimwa kwa ajili ya balbu zake. Hulimwa nyanda za baridi kwa wingi sana. Nyanda zenyewe joto Vitunguu kulimwa pia. Tanzania Vitunguu hulimwa sana sehemu za Mang'ula, Mgeta, na Singida. Hata hivyo vitunguu hustawi maeneo mengi ya Tanzania.

Vitunguu vinaweza kulimwa mwaka mzima endapo maji yanapatikana.

Vitunguu vina matumizi mengi sana na vina madini joto, chuma, vitamini A, vitamini B, vitamini C, na vitamini E.

HALI JOTO
Joto linatakiwa sana kwa ajili ya ukuaji wa balbu ila joto likizidi vitunguu hukomaa mapema kabla ya balbu hazijazifia ukubwa unaostahili, hivyo mkulima anaweza kupata mazao kidogo.

UDONGO NA MAHITAJI YA MAJI
Vitunguu huweza kupandwa kwenye udongo wowote wenye rutuba, usiotuamisha maji na usionata sana. Hufanya vizuri kwenye udongo wenye asidi kidogo hapo udongo wenye alkali kidogo sio mbaya sana. Kwenye udongo wenye mchanga mchanga umwagiliaji ni Lazima. Udongo mzuri sana kwa ustawi wa vitunguu ni tifutifu-kichanga.

Umwagiliaji ni muhimu sana hasa wakati wa kuanza kutengeneza balbu. Unyevu uliozidi ni hatari sana kipindi cha ukuaji.

Epuka matumizi ya mbolea mbichi isiyoiva vizuri Kwani husababisha vitunguu kuwa na shingo pana sana kipindi cha ukuaji.

UZALISHAJI NA UPANDAJI WA VITUNGUU
Kabla ya kupanda udongo ni Lazima utifuliwe vizuri na reki kuondoa mabaki ya mimea na mawe au kipande kikubwa vya udongo. Matuta yawe na upana wa mita moja. Vitunguu hupandwa kwa mstari moja kwa moja au kutokea kitaluni. Pia huweza kupandwa kwa mstari pacha. Vitunguu hupandwa sentimita 10-15 kutoka mmea hadi mmea na sentimita 10-15 kutoka mstari hadi mstari.

EPUKA
Kununua mbegu za mitaani, kuzidisha sana mbolea na umwagiliaji usio na mpangilio kwani husababisha vitunguu kuzaa pacha.
Epuka pia kupanda vitunguu mahali palipopandwa mboga jamii ya vitunguu siku za nyuma. Mfano vitunguu saumu au vitunguu majani.

KITALU CHA VITUNGUU
Ni muhimu kumwagilia maji ya kutosha siku kumi za mwanzo tangu kusia mbegu kitaluni. Vitunguu hukaa kitaluni kwa wiki 6-8 na miche ifikiapo upana wa penseli na urefu wa sentimita 15 ni tayari kwa kuhamishiwa shambani/bustanini.

AINA YA VITUNGUU VINAVYOLIMWA TANZANIA
. RED CREOLE
. BOMBAY RED
. HYBRID F1

UTUNZAJI SHAMBA
Kutandazia shamba na Majani yaliyooza vizuri ama mabua Inashauriwa ili kuongeza rutuba ya ardhi, Zuia magonjwa yatokanayo na udongo na magugu. Kupanda vitunguu kwenye matuta yaliyoinuka ni muhimu sana kuzuia utuamishaji wa maji na milipuko ya magonjwa ya miche. Kung'oa magugu na uvunaji ufanywe kwa mkono.

MAHITAJI YA MBOLEA
Vitunguu hufanya vizuri kama shamba litawekewa mbolea ya samadi ama mboji iliyoiva vizuri. Kiasi cha tani 25-40 kwa heka kina shauriwa. Hii ni sawa na kilo 7.5-12 kwa tuta lenye urefu wa mita 3 na upana wa mita 1

UVUNAJI
Vitunguu huvunwa kuanzia siku 90-150 tangu kusia mbegu. Dalili za kukomaa ni kuanguka kwa Majani. Vitunguu huvunwa kwa kuvuta kwa mkono na kuhifadhiwa siku kadhaa shambani vikiwa vimefunikwa na majani. Baada ya hapo majani hukatwa na balbu hupakiwa kwa ajili ya kuhifadhi kusubiria bei nzuri. Vitunguu huweza kuhifadhiwa hadi miezi 9 tangu vivunwe bila kuharibika. Vitunguu vihifadhiwe kwenye sehemu ya nyuzi joto chini ya 4.4°C ama juu ya nyuzi joto 25°C ili visiharibike.

UUZAJI
Vitunguu ni zao lenye bei nzuri ukilinganisha na mazao mengine ya mbogamboga na huuzwa kwenye masoko ya kawaida kwa bei nzuri kwa hivi sasa mwezi Septemba vitunguu  kilo moja ni shilingi 1,500/= kama vitunguu vikilimwa vizuri na kuhudumiwa ipasavyo. Hekari moja huzaa gunia 70-90 Sawa na 7,000-9,000kgs. Kama ukipata Soko la uhakika Mkulima anaweza kupata hadi milioni 13.5 kwa Msimu mmoja.

BUSTANI YA FREBU 
S.L.P. 77585, DSM, TANZANIA

Saturday, September 23, 2017

Karibu kwenye blog ya frebu media

Karibu kwenye blog ya Frebumedia blog. Blog hii inakupa habari za kweli na uhakika. Utapata habari za uhakika na matukio ya kila siku. Karibu sana frebumedia.blogspot.com blog yako ya kweli.


Ukiwa unataka kutangaza kwenye blog hii unakaribishwa. Tangaza kwa bei rahisi kuliko sehemu nyingine yoyote. Utalipia pesa ndogo sana kutangaza kwenye blog hii ys uhakika zaidi. Tunapokea matangazo  ya aina yoyote iwe kutangaza blog au kutangaza huduma au biashara. wasiliana nasi kwa email hii buberwamujuni@gmail.com utajibiwa na kuwekewa tangazo lako kwenye mtandao huu bira zaidi

Saidia kushare blog hii kwenye magroup ya whatsapp facebook twitter na kwingineko Ili mamilioni ya watu waje kusoma blog hii wapate habari za kweli na uhakika. Watumie anwani ya blog hii ambayo ni frebumedia.blogspot.com mtu akibonyeza link hiyo ataletwa kwenye blog hii.