MAELEZO YA MSINGI KUHUSU KILIMO CHA VITUNGUUMAJI
Vitunguu
ni zao la mbogamboga na hulimwa kwa ajili ya balbu zake. Hulimwa nyanda
za baridi kwa wingi sana. Nyanda zenyewe joto Vitunguu kulimwa pia.
Tanzania Vitunguu hulimwa sana sehemu za Mang'ula, Mgeta, na Singida.
Hata hivyo vitunguu hustawi maeneo mengi ya Tanzania.
Vitunguu vinaweza kulimwa mwaka mzima endapo maji yanapatikana.
Vitunguu vina matumizi mengi sana na vina madini joto, chuma, vitamini A, vitamini B, vitamini C, na vitamini E.
HALI JOTO
Joto
linatakiwa sana kwa ajili ya ukuaji wa balbu ila joto likizidi vitunguu
hukomaa mapema kabla ya balbu hazijazifia ukubwa unaostahili, hivyo
mkulima anaweza kupata mazao kidogo.
UDONGO NA MAHITAJI YA MAJI
Vitunguu
huweza kupandwa kwenye udongo wowote wenye rutuba, usiotuamisha maji na
usionata sana. Hufanya vizuri kwenye udongo wenye asidi kidogo hapo
udongo wenye alkali kidogo sio mbaya sana. Kwenye udongo wenye mchanga
mchanga umwagiliaji ni Lazima. Udongo mzuri sana kwa ustawi wa vitunguu
ni tifutifu-kichanga.
Umwagiliaji ni muhimu sana hasa wakati wa kuanza kutengeneza balbu. Unyevu uliozidi ni hatari sana kipindi cha ukuaji.
Epuka matumizi ya mbolea mbichi isiyoiva vizuri Kwani husababisha vitunguu kuwa na shingo pana sana kipindi cha ukuaji.
UZALISHAJI NA UPANDAJI WA VITUNGUU
Kabla
ya kupanda udongo ni Lazima utifuliwe vizuri na reki kuondoa mabaki ya
mimea na mawe au kipande kikubwa vya udongo. Matuta yawe na upana wa
mita moja. Vitunguu hupandwa kwa mstari moja kwa moja au kutokea
kitaluni. Pia huweza kupandwa kwa mstari pacha. Vitunguu hupandwa
sentimita 10-15 kutoka mmea hadi mmea na sentimita 10-15 kutoka mstari
hadi mstari.
EPUKA
Kununua mbegu za mitaani, kuzidisha sana mbolea na umwagiliaji usio na mpangilio kwani husababisha vitunguu kuzaa pacha.
Epuka pia kupanda vitunguu mahali palipopandwa mboga jamii ya vitunguu siku za nyuma. Mfano vitunguu saumu au vitunguu majani.
KITALU CHA VITUNGUU
AINA YA VITUNGUU VINAVYOLIMWA TANZANIA
. RED CREOLE
. BOMBAY RED
. HYBRID F1
UTUNZAJI SHAMBA
Kutandazia
shamba na Majani yaliyooza vizuri ama mabua Inashauriwa ili kuongeza
rutuba ya ardhi, Zuia magonjwa yatokanayo na udongo na magugu. Kupanda
vitunguu kwenye matuta yaliyoinuka ni muhimu sana kuzuia utuamishaji wa
maji na milipuko ya magonjwa ya miche. Kung'oa magugu na uvunaji ufanywe
kwa mkono.
MAHITAJI YA MBOLEA
Vitunguu
hufanya vizuri kama shamba litawekewa mbolea ya samadi ama mboji
iliyoiva vizuri. Kiasi cha tani 25-40 kwa heka kina shauriwa. Hii ni
sawa na kilo 7.5-12 kwa tuta lenye urefu wa mita 3 na upana wa mita 1
UVUNAJI
Vitunguu
huvunwa kuanzia siku 90-150 tangu kusia mbegu. Dalili za kukomaa ni
kuanguka kwa Majani. Vitunguu huvunwa kwa kuvuta kwa mkono na
kuhifadhiwa siku kadhaa shambani vikiwa vimefunikwa na majani. Baada ya
hapo majani hukatwa na balbu hupakiwa kwa ajili ya kuhifadhi kusubiria
bei nzuri. Vitunguu huweza kuhifadhiwa hadi miezi 9 tangu vivunwe bila
kuharibika. Vitunguu vihifadhiwe kwenye sehemu ya nyuzi joto chini ya
4.4°C ama juu ya nyuzi joto 25°C ili visiharibike.
UUZAJI
Vitunguu
ni zao lenye bei nzuri ukilinganisha na mazao mengine ya mbogamboga na
huuzwa kwenye masoko ya kawaida kwa bei nzuri kwa hivi sasa mwezi
Septemba vitunguu kilo moja ni shilingi 1,500/= kama vitunguu vikilimwa
vizuri na kuhudumiwa ipasavyo. Hekari moja huzaa gunia 70-90 Sawa na
7,000-9,000kgs. Kama ukipata Soko la uhakika Mkulima anaweza kupata hadi
milioni 13.5 kwa Msimu mmoja.
BUSTANI YA FREBU
S.L.P. 77585, DSM, TANZANIA
EmoticonEmoticon