USINDIKAJI WA PAPAI
Papai ni mojawapo ya mazao ya matunda yenye vitamini A na madini ya kalishamu kwa kiasi kikubwa sana.
Zao
Hili hustawi kila mahali nchini Tanzania. Kwa mwaka, wastani wa tani
2,580 hadi mwaka 2016, huzalishwa kote nchini, na uzalishaji wa zao hili
unaongezeka kila msimu kulingana na uhitaji.
Matunda husindikwa ili kupata bidhaa za aina mbalimbali kama vile jamu, na matunda makavu.
NAMNA YA KUSINDIKA PAPAI ILI KUPATA JUISI
Mahitaji:
Visu vikali visivyoshika Kitu
Vyombo vya kuoshea matunda
Mashine ya Kusaga matunda
Kipimo cha Sukari
Chupa zenye mifuniko imara
Saa
Nembo na lakiri
Kipima joto
Sufuria
Jiko
Mwiko
Vitambaa au chujio
MALIGHAFI KWA AJILI YA KUTENGENEZA LITA 3 ZA JUISI
MAPAPAI mawili ya ukubwa wa kati
Sukari gramu 100
Juisi ya limao/ndimu kikombe cha Chai kimoja
Maji safi na salama Lita 3
NAMNA YA KUSINDIKA
Osha matunda kwa maji safi na salama
Menya kuondoa Mabanda na mbegu
Katakata vipande vidogo vidogo, kisha saga kwa kutumia mashine ili kupata rojo.
Ongeza
maji ya limao au ndimu ili kupata ladha. Katika Kila Lita 1 ya rojo ya
mapapai weka kikombe kimoja cha Chai cha Juisi ya limao au ndimu ili
kuongeza ladha na kuboresha uhifadhi. Ongeza maji safi kiasi cha Lita 3.
Chuja kwa kutumia chujio safi.
Chemsha mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 20 ukiwa unakoroga katika joto la nyuzi 80°C hadi 90°C
Ipua
Weka Juisi kwenye chupa safi zilizochemshwa Ikiwa na moto kisha funga kwa mifuniko imara.
Panga chupa kwenye sufuria kisha weka weka maji kufikia nusu ya kimo cha chupa.
Chemsha chupa kwa muda wa dakika 20 ili kufisha bakteria na vimelea vinginevyo.
Ipua chupa na acha zipoe
Weka nembo
Hifadhi katika sehemu safi yenye hali ya joto lisilozidi nyuzi 25°C na isiyo na mwanga mkali.
MATUMIZI
Juisi hutumika kama kinywaji au kiburudisho na ina virutubisho vya vitamini C na A kwa wingi
USINDIKAJI WA MAPAPAI KWA KUKAUSHA
Mahitaji:
Kaushio bora
Mashine ya kufungia, au jiko la mkaa, au mishumaa.
Meza safi ya Kukutia
Kisu kisichoshika Kitu
Beseni la kuoshea
Mifuko ya plastiki au chupa ya plastiki au kioo.
MALIGHAFI
Mapapai yaliyoanza kuiva
Maji ya malimao au ndimu
JINSI YA KUTENGENEZA
Osha mapapai yaliyoiva vizuri na yasiyo na magonjwa wala mikwaruzo.
Menya kwa kutumia kisu kikali kisichoshika kutu.
Katakata
kwenye kipande visivyozidi urefu wa sentimita 10 na Unene wa milimita
3. Ujizidisha ukubwa wa vipande havitakauka vizuri na kusababisha ubora
wake kushuka.
Viweke vipande hivyo ndani ya maji ya malimao au ndimu kwa muda wa dakika 1 hadi 2 ili kudumisha rangi papai na kuongeza ladha.
Panga vipande kwenye trei za kaushio
Kausha kwa muda wa siku 3 hadi 4 kutegemeana na hali ya jua.
Fungasha kwenye mifuko ya plastiki au chupa za kioo safi na uhifadhi kwenye sehemu kavu nyenye mwanga hafifu na safi.
MATUMIZI YA PAPAI
Papai lililoiva
Huliwa kama tunda
Hutengenezwa Jamu na Juisi
Hukaushwa na Kuliwa kwa kuchanganywa wenye saladi ya matunda au keki.
Hutia ladha kwenye ice cream
Papai bichi
Utomvu wa papai bichi, hutumika katika matumizi yafuatayo;
Kutengeneza peremende, dalia, urembo, na madawa ya kulainisha Tumbo.
Huwekwa kwenye nguo wakati wa kutengenezwa ili isifupike.
Hulainisha nyama.
Hulainisha ngozi.
Papai bichi pia hutengenezwa
Mboga
Achari
EmoticonEmoticon